FDA News Release
FDA Inawaonya watumiaji kuhusu madhara hatari na yanayoweza kutokea ya Miracle Mineral Solution (Mmumunyo wa Madini ya Miujiza)
- For Immediate Release:
Usimamizi wa Chakula na Dawa Marekani (U.S. Food and Drug Administration) unawaonya watumiaji kutonunua wala kutokunywa bidhaa inayouzwa mtandaoni kama matibabu kwa sababu ya ongezeko la masuala ya kiafya yaliyoripotiwa. Tangu 2010, FDA imewaonya watumiaji kuhusu hatari za Miracle or Master Mineral Solution, Miracle Mineral Supplement, MMS, Chlorine Dioxide (CD) Protocol, Water Purification Solution (WPS) na bidhaa nyingine kama hizo. Miracle Mineral Solution haijathibitishwa na FDA kwa utumiaji, lakini bidhaa hizi zinazidi kupigiwa debe kwenye mitandao ya kijamii kama dawa ya kutibu otizimu, saratani, UKIMWI, hepatitis na mafua. Hata hivyo, mmumunyo, ukichanganywa, hufanyika dawa hatari ya klorini ambayo imesababisha madhara mabaya sana na yanayotishia maisha.
“Mchakato wa FDA wa kuidhinisha dawa huhakikisha kwamba wagonjwa hupata bidhaa za dawa salama na za kufanya kazi. Miracle Mineral Solution na dawa nyingine kama hizo hazijaidhinishwa na FDA na kutumia bidhaa hizi ni sawa na kutumia dawa za klorini. Watumiaji hawafai kutumia bidhaa hizi, na wazazi hawafai kupeana bidhaa hizi kwa watoto wao kwa sababu yoyote,” alisema Kamishna Anayeshikilia wa FDA Ned Sharpless, M.D. “FDA itaendelea kuwafuatilia wanaouza bidhaa hii hatari na kuchukuwa hatua zifaazo za kisheria dhidi ya wale wanaojaribu kukwepa masharti ya FDA na kupigia debe bidhaa ambazo hazijaidhinishwa na ambazo ni hatari kwa umma wa Marekani. Kipaumbele chetu cha juu ni kulinda umma dhidi ya bidhaa zinazoweka afya yao kwenye hatari, na tutatuma ujumbe mkali na wa wazi kwamba bidhaa hizi zina uwezo wa kusababisha hatari kubwa.”
Tovuti zinazouza MMS huelezea bidhaa kama kiowevu kilicho na 28% ya kloridi ya sodiamu katika maji. Maelekezo ya bidhaa huwaagiza watumiaji kuchanganya mmumunyo wa kloridi ya sodiamu kwa asidi ya citric – kama vile ndimu au sharubati la limau – au asidi nyingine kabla ya kunywa. Katika matukio mengi, kloridi ya sodiamu huuzwa na asidi ya citric “kichochezi.” Wakati asidi inaongezwa, mchanganyiko hufanyika dayoksidi ya kloridi, kiyeyushaji chenye nguvu.
FDA hivi majuzi ilipokea ripoti mpya ya watu wanaopitia kutapika kubaya, kuhara kubaya, shinikizo la damu dogo sana la kutishia Maisha linalosababishwa na mwili kupoteza maji na kukosa kufanya kazi kighafla kwa maini baada ya kunywa bidhaa hizi. FDA haifahamu Ushahidi wowote wa kisayanzi unaotoa msingi wa usalama au ufanisi wa bidhaa za MMS, licha ya madai kwamba mmumunyo ni wa antimicrobial, antiviral na antibacterial. FDA inahimiza watumiaji kuzungumza na mtaalamu wa huduma za afya kuhusu kutibu hali za kimatibabu au magonjwa.
Watumiaji waliopitia madhara makali ya kiafya baada ya kutumia bidhaa hii wanafaa kutafuta matibabu ya haraka. Yeyote aliyepata athari mbaya ya kiafya ambayo inaweza kuwa na uhusiano na MMS anafaa kuripoti kupitia mpango wa FDA wa Habari ya Usalama wa MedWatch (MedWatch Safety Information program) haraka iwezekanavyo kwa 800-FDA-1088 au www.fda.gov/medwatch/report.htm.
FDA, shirika katika Idara ya Afya na Huduma kwa Watu ya Marekani, hulinda afya ya umma kwa kuhakikisha usalama, ufanisi, na ulinzi wa dawa za binadamu na za mifugo, chanjo na bidhaa nyingine za kibayolojia kwa utumiaji wa binadamu, na vifaa vya kimatibabu. Shirika pia linawajibikia usalama na ulinzi wa usambazaji wa chakula katika nchi yetu, vipodozi, virutubisho vya lishe, bidhaa zinazotoa miale ya kielektroniki, na kudhibiti bidhaa za tumbaku.
Related Information
###
Inquiries
- Media:
- Gloria Sánchez-Contreras
- (301) 796-7686
- Consumer:
- 888-INFO-FDA