U.S. flag An official website of the United States government
  1. Home
  2. For Consumers
  3. Consumer Updates
  4. Hatari: Usikunywe Miracle Mineral Solution au Bidhaa kama Hizo
  1. Consumer Updates

Hatari: Usikunywe Miracle Mineral Solution au Bidhaa kama Hizo

Image
Five plastic bottles labeled with "Miracle Mineral Solution" and similar product names followed by an equal sign and a bottle labeled "Chlorine Dioxide - Powerful Bleaching Agent"

English

Iwapo unakunywa “Miracle” au “Master” Mineral Solution au bidhaa nyingine ya kloridi ya sodiamu, acha sasa .

FDA (The U.S. Food and Drug Administration) imepokea ripoti nyingi kwamba bidhaa hizi, zinazouzwa mtandaoni kama “matibabu,” zimewafanya watumiaji kugonjeka.

FDA kwanza iliwaonya watumiaji kuhusu bidhaa katika mwaka wa 2010. Lakini bado zinapigiwa debe kwenye mitandao ya kijamii na kuuzwa mtandaoni na wasambazaji huru wengi. Shirika linawaomba watumiaji kutonunua wala kutumia bidhaa hizi.

Bidhaa zinajulikana kwa majina mengi, ukijumuisha Miracle au Master Mineral Solution, Miracle Mineral Supplement, MMS, Chlorine Dioxide (CD) Protocol, na Water Purification Solution (WPS). Zikichanganywa kulingana na maelekezo kwenye pakiti, zinafanyika kemikali kali ambayo inatumika kama dawa ya klorini.

Wasambazaji wengine wana madai— ya uwongo—na hatari kwamba Miracle Mineral Supplement ikichanganywa na asidi ya citric inafanyika antimicrobial, antiviral, na kiowevu cha antibacterial ambacho ni dawa ya otizimu, saratani, UKIMWI, hepatitis, mafua, na hali nyinginezo. Lakini FDA haina ufahamu wa utafiti wowote unaoonyesha kwamba bidhaa hizi ni salama au fanisi kwa kutibu ugonjwa wowote. Kutumia bidhaa hizi kunaweza kukusababisha kuchelewesha matibabu mengine ambayo yameonyeshwa kuwa salama na fanisi.

Ukweli ni kwamba: Bidhaa za kloridi ya sodiamu ni hatari, na wewe na familia yako hamfai kuzitumia.

Watumiaji wa MMS Consumers Wanakunywa Dawa ya Klorini

Tovuti zinazouza Miracle Mineral Solution huelezea bidhaa kama kiowevu ambacho kina asilimia 28 ya klorini ya sodiamu kwa maji. Maelekezo ya bidhaa huwaagiza watu kuchanganya mmumunyo wa kloridi ya sodiamu na asidi ya citric, kama vile ndimu au sharubati la limau, au asidi nyingine kabla ya kunywa. Katika matukio mengi, kloridi ya sodiamu huuzwa na asidi ya citric “kichochezi.” Asidi ikiongezwa, mchanganyiko hufanyika dayoksidi ya klorini, dawa kali ya klorini.

Kloridi ya sodiamu na dayoksidi ya kloridi ni viungo amilifu katika viua viini na vina matumizi zaidi ya viwandani. Havijaundwa kumezwa na watu.

Suluhisho la Madini ya Muujiza husababisha Rejea Mbaya

Kunywa bidhaa yoyote ya dayoksidi ya kloridi kunaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, kuhara, na ishara kali za kupoteza maji mwilini. Baadhi ya vibandiko vya bidhaa vinadai kwamba kutapika na kuhara ni kawaida baada ya kunywa bidhaa. Hata wanadumisha kwamba ishara kama hizo ni thibitisho kwamba bidhaa inafanya kazi. Dai hilo ni la uwongo.

Zaidi ya hayo, kijumla, bidhaa inavyoshikana zaidi, ndivyo athari zinavyokuwa hatari zaidi. FDA imepokea ripoti za watumiaji ambao wameumia sana kwa kutapita sana, kuhara sana, shinikizo la damu dogo la kutishia maisha linalosababishwa na kupoteza maji mwilini, na kukosa kufanya kazi kighafla kwa maini baada ya kunywa bidhaa hizi. Iwapo umekuwa na athari mbaya kwa yoyote, shauriana na mtaalamu wa huduma ya afya kwa haraka iwezekanavyo.

Wataalamu wa huduma za afya na wagonjwa wanahimizwa kuripoti matukio mabaya au athari zinazohusiana na utumiaji wa bidhaa hizi kwa Mpango wa MedWatch wa FDA wa Kuripoti Tukio Baya na Habari Ya Usalama (FDA's MedWatch Safety Information and Adverse Event Reporting Program):

SUBSCRIBE

Get regular FDA email updates delivered on this topic to your inbox.

Back to Top